Mpango Kambambe jiji la arusha

Mpango kabambe wa Jiji la Arusha unatekelezwa na Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Singapore. Mpango huu unajulikana kama Arusha City Master Plan 2035.

Katika Tanzania Mpango huu unatekelezwa kwenye majiji mawili ikiwemo Jiji la Arusha na Jiji la Mwanza na ulianza mwaka 2014 kwa kufanya tafiti mbali mbali juu ya Ardhi na Makazi na ni mpango wa muda mrefu mpaka mwaka 2035.

Mpango kabambe wa Jiji la Arusha unategemea kutekelezwa katika Halmashauri ya Arusha kwa eneo la kilomita za mraba 149 katika baadhi ya maeneo ya kata za Oloirieni, Kimnyaki, Bangata, Moivo, Mlangarini, Kiranyi, Kiutu, Sokoni II, Ilboru na Matevesi.

Mpango kabambe wa Jiji la Arusha unalenga kupanga Mji wa Arusha kwa kuzingatia maeneo halisi, Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, ukuaji wa kasi wa miji, maeneleo ya kiuchumi, mahitaji ya jamii pamoja na ongezeko la watu katika ardhi hii isiyoongezeka.

Mpango huu umepanga maeneo ya makazi, maeneo ya huduma za Jamii kama shule, viwanja vya wazi, maeneo ya Viwanda, maeneo ya Kilimo na mifungo, maeneo ya biashara ndogo ndogo n.k.

Matangazo